Kuhusu sisi

Chuo cha Africa Academy kimebuniwa kwa lengo la kuwasaidia wazungumzaji wa Kiswahili kuelewa kwa usahihi dini ya Uislamu kupitia Qur’an Tukufu na Sunnah za Mtume Muhammad ﷺ.
Ni jukwaa la kimtandao (kidigitali) linalotoa programu ya kielimu inayolenga kuleta watu karibu na elimu ya Kiislamu kwa njia rahisi kupitia: mtandao wa intaneti (wavuti), mitandao ya kijamii na chaneli za Afrika TV.
Jukwaa hili limechagua mfumo wa elimu huria kwa njia ya kozi fupi (MOOCs – Massive Open Online Courses) ili kila mtu mwenye nia ya kujifunza aweze kushiriki kwa urahisi.
Africa Academy hufanya kazi mtandaoni kwa 100% – wanafunzi wanaweza kuingia kwenye kozi kwa kutumia kompyuta au simu janja, na kuhudhuria masomo kwa sauti, video au vitabu vya kielektroniki, na kujibu maswali ya kujipima.
Africa Academy inategemea walimu mahiri na maarufu kutoka miongoni mwa wahubiri (maduat) wa Ahlus-Sunna wal-Jama’a wanaozungumza lugha ya Kiswahili.

Maono

Tunatarajia katika awamu tatu za kwanza kushirikisha wanufaika 30,000 kupitia mfumo wa elimu huria.

Ujumbe

Africa Academy iwe taasisi ya kielimu inayoongoza katika elimu ya mtandaoni kwa lugha za Kiswahili, kwa kutumia mbinu za kisasa na teknolojia bora, kupitia matangazo ya televisheni ya satelaiti na majukwaa mbalimbali ya intaneti.

Malengo

1 – Kuziba haja ya Waislamu juu ya misingi ya elimu ya Kiislamu na kile ambacho mtafutaji wa elimu (mwanafunzi) hapaswi kutokujua kwa lugha za Kiafrika.
2 – Kueneza itikadi ya Ahl al-Sunnah wal-Jama’ah na Fiqh sahihi kwa ushahidi wake kutoka kwa Qur’an na Sunnah.
3 – Kumfundisha mwanawake wa Kiislamu dini yake, kuongeza uelewa wake na kumuelimisha, na kuchangia katika maandalizi ya wanafunzi wa kike wa elimu ya Kiislamu.
4 – Kueneza utamaduni wa kujifunza elimu za Sharia kwa njia ya mtandao barani Afrika kwa kutoa mtaala wa kielimu ambao unazingatia utaalam na uvumbuzi katika mbinu za uwasilishaji.