Kozi Fupi ya hukumu za Swaumu ya Ramadhani:
Baada ya kumaliza kozi, mwanafunzi anaweza kujua ni nani anawajibika kufunga, kufunga ipasavyo na kuepuka kila aina ya mambo yanayoharibu Swaumu kwa aina zote, na kujua ni kwa nani inajuzu kufuturu katika mwezi wa Ramadhani na kwa nini?
Yale ambayo yanamlazimu au wajibu kwake baada ya kufuturu, na atazifahamu vyema fadhila za Ramadhani na Laylat Al-Qadr na ni Kauli za wanachuoni sahihi zinazofafanua hayo, na atafahamu idadi ya adabu na sunna wakati wa kufunga.
Kozi hii imewasilishwa na Sheikh: Muharram Idris Muita
Kuanzia tarehe 26Feb hadi 5 Machi 2025.